WE ARE FAMILY

Welcome in in our family

WE ARE SERVICE

We meets weekly every thursday from 5pm at WalkGuard hotel/transit

Monday 13 February 2017

A VISIT TO NTOMA ORPHANAGE

The Ntoma Orphanage was founded in 1953 by the ELCT.
It caters for babies and children of ages 0 to 1 and a half
It has the capacity of up to 30 babies and has 16 staff.
The Rotaract Club of Bukoba delivered donations of Maize flour, Beans, Cooking oil, Soap and tshirts.

No automatic alt text available.Image may contain: outdoorImage may contain: one or more peopleImage may contain: indoorImage may contain: 4 people, people smiling, people standing, shoes and outdoorImage may contain: 3 people, outdoorImage may contain: grass and outdoorImage may contain: 1 person, sitting and indoorImage may contain: sky, grass, house, outdoor and natureImage may contain: house, grass, tree, sky, plant, outdoor and natureImage may contain: house and outdoorImage may contain: bedroom and indoorImage may contain: 4 people, people smiling, people standingImage may contain: one or more people and people sleepingNo automatic alt text available.Image may contain: one or more people and people sittingImage may contain: one or more peopleImage may contain: 1 person, sittingImage may contain: one or more peopleImage may contain: one or more people, people sleeping, baby and indoorImage may contain: one or more peopleNo automatic alt text available.No automatic alt text available.

Saturday 3 September 2016

DAWA ZA KULEVYA NA ATHARI ZAKE

Friday 2 September 2016

UKWELI KUHUSU UGONJWA WA UTI :ATHARI KINGA NA MATIBABU YA UGONJWA WA UTI.

Asilimia kubwa ya Watanzania hawaujui vizuri ugonjwa wa UTI. Kumekwepo na maelezo kutoka kwa watu mbali mbali na wakati mwingine hata kwa wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa huu lakini bado watu wengi wanakanganyika na ukweli halisi.Leo nitajaribu kutoa maelezo walau kwa kina ili jamii iujue ugonjwa huu kinagaubaga.

Kwanza kabisa kirefu cha cha herufi UTI ni URINARY TRACT INFECTION ikimaanisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.

Msomaji anapaswa kujua njia ya mkojo ni ipi, inaanzia wapi na inaishia wapi. Kwa ujumla njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa mwanaume na mwanamke. Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS.Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu.Wanawake wanakua na urethra fupi 4cm kulinganisha na wanaume 25cm hivo kupelekea kupata UTI kwa urahisi.



Kibofu kikipata maambukizi ugonjwa unajulikana kama CYCITITIS. Baada ya kibofu inafuata mirija miwili inayokwenda kwenye figo mbili. Mirija hii inaitwa URRETERS na ikishaambukizwa inajulikana kama URRETITIS.Na mwisho wa njia ya mkojo ni figo mbili yaani KIDNEYS na hizi figo zikishaambukizwa ugonjwa unajulikana kama NEPHRITIS.


Hivyo sababu huambatana na chanzo cha tatizo katika mojawapo ya sehemu husika, Mfano:
1. Ugonjwa wa sukari hufanya kiwango cha sukari kuwa kikubwa kwenye damu kwa vile mafigo kazi yake ni kuchuja damu hivyo ni kusema sukari huingia kwa wingi kiasi cha kusababisha vidudu bakteria kuzaliana kwa wingi kwenye mafigo au kibofu cha mkojo.

2. Madawa /sumu huchubua utando wa njia ya mkojo na kusababisha bacteria kuzaliana

3. Matatizo ya vijiwe kwenye figo/ mirija ya mkojo, kibofu, hufanya msongomano wa mkojo na Vijidudu huzaliana.

4. Maradhi ya Tunda Prostate gland huvimba na kufunga njia ya mkojo matokeo yake kuuzuia na kuuweka mkojo mda mrefu kwenye kibofu mpaka bacteria kuzaliana.
5. Tendo la ndoa, sexual intercouse unapata vijidudu moja kwa moja kutoka kwa mwanamke mwenye uambukizo

6. Kujichua, tendo hili mara nyingi watu hutumia mafuta au sabuni ambazo huwa zina kemikali zinazopenya kwenye mrija wa mkojo huwasha na kusababisha vidonda ambayo bacteria hukua na kazaliana

7. Usafi, aidha kwa kujikamua sana baada kukojoa, kutawaza maji machafu kutokuwa na hali ya unadhifu, huko chini kuna vijidudu ambavyo huishi baina ya njia ya haja kubwa na makorodani kutokana na hali ya ujoto humea vizuri na hupata nafasi ya kukuingia kwenye mirija kama utakuwa huna tabia ya kuwapunguza kwa usafi.


Sasa basi ni lazima tujue ni vimelea wa aina gani wanaoleta ugonjwa wa UTI.


Hapa nitajaribu kuonisha na kupanga vimelea katika makundi maalum.
Vimelea vinavyojulikana ni kama ifutavyo:
1. BACTERIA eg Streptococci, Staphylococci, E.Coli, H.Influenza, Proteus sp.Pseudomonas etc.
2. VIRUSES eg Clamydia tracomatis
3. FUNGI eg Candida albicans
4. TRICHOMONIASIS
5. SCHISTOSOMIASIS (kichocho)
6. PARASITES
7. GONORRHEA (kisonono).

Watoto wadogo mara nyingi wanapata UTI kutokana na kutobadilisha nepi kwa wakati na hivyo unyevu wa mikojo na mavi huvuta vimelea na kuleta maambukizi. Kwa watu wazima hasa wale wanaofanya ngono zembe wanapata magonjwa ya zinaaa kwa urahisi na hivyo wanakuwa tayari wana UTI. Kuna fikra kubwa imejengeka miongoni mwa jamii kuwa UTI inaletwa kwa urahisi kwenye vyoo vya kuchangia.


Image result for African baby in diapers
Dhana hii kwangu naweza kusema si sahihi hata kidogo kwa sababu wanaume wanakojoa kwa kuagiza mkojo kwa mbali kama risasi kwenye tundu la choo, sasa hao vimelea wanafuata mkondo wa mkojo kama unavyofanya umeme? Au wanaruka na kuja kuingia kwenye tundu la mkojo? Jibu ni hapana.Kwa wanawake wao wanajisaidia kwa kuchuchamaa, lakini hii sio sabau kua nyeti zao zinagusa kwenye sinki au shimo la choo na wala vimelea vya magonjwa vilivyomo chooni haviambukizi kamwe kwa ya mvuke.

Dalili za UTI zinaonekana kulingana na aina ya maambukizi.Lakini dalili kuu kwa watoto na watu wazima zinafanana nazo ni maumivu wakati wa kukojoa na pengine kutoka uchafu au usaha kwenye njia ya mkojo.Hizi ni dalili za UTI kulingana na aina ya maambukizi.Kama nilivotangulia kusema awali zipo aina tatu za UTI urethritis(maambukizi kwenye mrija wa mkojo),cystitis (maambukizi kwenye kibofu) na pyelonephritis(maambukizi kwenye figo)


 Urethritis dalili zake ni kupata maumivu wakati wa kukojoa
cystitis dalili zake ni kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu na saa nyingine kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu.
Pyelonephritis dalili zake ni Homa,kichwa kuuma,kichefuchefu,kutapika,maumivu ya tumbo sehemu za pembeni na mgongo kuuma.

MATIBABU:UTI ni ugonjwa unaotibika kabisa,pindi utapopata dalili hizi unashauriwa kufika hospital na kupata vipimo na matibabu sahihi.


JINSI YA KUJIKINGA NA UTI:
Eneo hili ni muhimu sana,watu wengi wamekua wakidhania kua UTI haiponi kutokana na sabau kua wamekua wakipata tena uti muda mfupi baada ya matibabu,ni kwa sabau watu hawazingatii jinsi gan ya kujikinga na ugonjwa huu.Hizi ni njia za kujikinga
Jisafishe kutokea mbele kwenda nyuma:Hii ndio sabau kubwa ya wanawake kupata UTI kwasababu wakati wa kujisafisha baada ya haja kubwa wanasafisha kwa kuvuta maji kutoka nyuma kwenda mbele ambapo wanabeba bacteria waliopo kwenye njia ya haja kubwa na kuwaleta kwenye njia ya haja ndogo hivo kupata maambukizi.



Vaa nguo za ndani zinazoweza kufyonza unyevunyevu sana sana nguo za cotton

Kunywa maji ya kutosha,Inashauriwa mtu kunywa angalau lita 2 na nusu kwa siku.
Pia unashauriwa kukojoa baada ya tendo la ndoa hii husaidia kutoa nje vijidudu vilivoingia kwenye mrija wa mkojo wakati wa tendo

Wednesday 22 June 2016

ROTARACT HANDBOOK:ALL YOU NEED TO KNOW ABOUT ROTARACT

Dear Rotaractors you can download the rotaract Hand book here to learn more about Rotaract.



Wednesday 25 November 2015

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu

Kwa kua Ugonjwa wa kipindupindu umekua ukienea kwa kasi sana na kufika katika Manispaa ya mji wetu wa Bukoba.Rotaract club of Bukoba inapenda kukumbushana na jamii kuhusu njia za kujikinga na Ugonjwa huu hatari wa kipindupindu na kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huu katika Mji wetu na Tanzania nzima.

Kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria aina Vibrio cholera. Ugonjwa huu ni moja ya magonjwa ya nayoiathiri jamii hasa pale unapotokea kwani ni miongoni mwa magonjwa ya milipuko.
Ugonjwa huu uambukizwa kutokana na vimelea vinavyopendelea kuishi kwenye kinyesi cha binadamu. Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa kwa kunywa maji au kula chakula kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea vya kipindupindu.

baada ya mtu kula chakula au kunywa kinywaji chenye vimelea vya kipindupindu, baadhi ya vimelea huuawa kwa tindikali iliyopo kwenye utumbo pindi chakula au maji hayo yanapoingia tumboni.
Hata hivyo baadhi ya vimelea hufanikiwa kukwepa tindikali hiyo na kuendelea kuishi. Vimelea hivyo vilivyofanikiwa kukwepa tindikali hiyo hujishikisha kwenda kwenye ukuta wa utumbo mdogo kwa kutumia maumbo maalum yaliyomo kwenye mwili wa binadamu ambayo huwezesha kusafiri ambayo kwa kitaalamu huitwa flagella.
Vimelea hivyo viwapo kwenye utumbo mdogo hutoa sumu iitwayo CTX au CT(cholera toxin) ambapo sumu hiyo husababisha mtu kuhara choo chenye majimaji. Licha ya kutoa sumu hiyo pia huendelea kutoa kizazi kingine cha vimelea hao nje kwa njia ya haja kubwa.
Iwapo choo hicho cha mtu aliyeambukizwa kipindupindu kitachanganyika na chanzo chochote cha maji au chakula watu wengine huweza kuambukizwa kipindupindu.

Maambukizi yake
Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya Vibrio cholerae zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya mchele.
Kipindupindu hutokea hasa pale mazingira yanapokuwa sio safi kwa kiasi kikubwa kwani maji, vyakula, hata vyoo huweza kuwa katika hali ya uchafu.
Bakteria ya vibrio cholerae hupatikana hasa katika kinyesi na maji ya choo na pia katika maji ya bahari, maziwa na mito kama maji machafu huingizwa katika magimba ya maji bila kusafishwa kwanza.
Katika mazingira yenye maji ya bomba, yaliyosafishwa na karakana ya kusafisha maji machafu, kipindupindu hutokea mara chache sana.

Dalili zake
Dalili za awali za kipindupindu ni pamoja na kuhara ghafla choo chenye majimaji (kinakuwa na maji kama ya maji ya mchele) na choo hicho muda mwingine huwa na harufu kali kama shombo ya samaki.
Kutapika .Pia mgonjwa huonyesha dalili za kupungukiwa na maji mwilini kama vile ngozi kuwa kavu, midomo kukauka, mgonjwa kuhisi kiu kikali, kupata mkojo kidogo sana. Pia mgonjwa huwa na homa kali.
Kuishiwa nguvu na kujisikia mchovu sana pamoja na macho kutumbukia ndani hasa kwa watoto
Jinsi ya kutambua ugonjwa huu
Ugonjwa huu huweza kugunduliwa na kutambuliwa kwa kuona dalili zake. Hata hivyo ili kudhibitisha kuwa kama dalili alizonazo mgonjwa zinatokana na ugonjwa huo vipimo vifuatavyo huweza kutumika kuwa na uhakika zaidi.
Mgonjwa huweza kupimwa damu kwa hajili ya kuotesha vimelea vya kipindupindu katika maabara.
Pia choo cha mgonjwa huweza kuchunguzwa kwa kutumia darubini(dark field microscope) ambapo kama ugonjwa ni wenyewe vimelea huweza kuonekana.

Tiba
Mgonjwa wa kipindupindu huweza kupatiwa matibabu huku lengo kuu likiwa ni kurejesha maji na madini mwilini aliyoyatoa kwa njia ya kuhara au kutapika.
Njia itumikayo kumpatia maji hayo ni kwanjia ya mdomo ambapo hupewa anywe au kwanjia ya mshipa wa damu ambayo kitaalamu hujulikana kama intravenously(i.v)
Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa sababu mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya kwa njia ya kuhara na kutapika.
Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone.


Jinsi ya kujikinga na kipindupindu
  1. Miongoni mwa njia zinazoweza kusaidia kuepuka na kupatwa na ugonjwa huu ni pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.Watu wengi wanatakiwa kuhakikisha wanapata maji safi na salama huku kabla ya kunywa maji hayo wanahakikisha wameyachemsha na kuyachuja pamoja na kuyahifadhi kwenye chombo safi.
  2. Ni muhimu kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kila mara baada ya kutoka chooni ili kuepuka kula au kushika chakula chochote huku mikono ikiwa michafu.
  3. Pia jamii inashauriwa kufunika chakula kikiwa mezani ili nzi wasiweze kutua juu yake
  4. Licha ya kuzingatia usafi pia inashauliwa kujenga choo angalau mita 30 kutoka kilipo chanzo cha maji pamoja na kuweka mazingira katika hali ya usafi kwa ujumla.
  5. Ili kuweza kuepuka ugonjwa Dk Chirwa anasema kuwa jamii inatakiwa kuzingatia usafi ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi na salama kwa kutumia sabuni. Hii ni muhimu sana hasa kwa watoto wanapokuwa shuleni ili kuepuka kupatwa na ugonjwa huo.
  6. Pia ni muhimu kunawa kabla ya kuandaa chakula au kula huku ukizingatia usafi wa vyombo vinavyotumika kuandalia chakula au kulia chakula hicho.
  7. Kusafisha matunda kwa maji safi na salama hasa ya uvuguvugu kabla ya kuyamenya au kuyala kwa yale yasiyohitaji kumenywa.
  8. Kufunika chakula ili kuepusha uwezekano wa wadudu hasa nzi kutua juu ya chakula hicho kwani wanaweza kuacha baktelia wanaoweza kuwa wamewabeba kwenye miguu yao.
  9. Maji ya choo yanayotokana na wagonjwa wa kipindupindu yanapasa kupitia mashimo ya choo yaliyohifadhiwa vizuri ili kuzuia usambazaji wa bakteria
  10. Vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto
  11. Mikono inayoshika wagonjwa au nguo zao inapaswa kusafishwa kwa maji na sabuni
  12. Mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia klorini

Saturday 31 October 2015

WHAT THE ROTARY EMBLEM(WHEEL) MEANS

Here is some background on how the logo was developed and what it means.
Back in 1905, an engraver and Chicago Rotarian, Montague Bear, designed a simple Rotary wagon wheel, showing movement and dust. It was meant to represent civilization, movement and service work in action. Over time, many Rotary clubs adopted the wheel in one form or another.

In 1922 it was decided to create and develop an official Rotary emblem and in 1923 a gear with 24 teeth and six spokes was officially adopted. To me, the gear teeth around the outside represent the fact that work is to be done.

The six spokes represent the inner direction and path of our Vocational Service, through the representation of our membership via the classification system. Similarly, these same spokes represent an outward distribution path of Rotary's ideals of service and the Four Way Test… going out toward the community, vocations and businesses that our members represent.
At the 1929 Rotary International Convention, it was determined that blue and gold would be the official colors of the organization, so the wheel was designed with these colors. The four blue bands within the outer radius of the gear represent our four avenues of service.

Some time later, Rotarian engineers pointed out that a gear could not be effective just turning freely on a shaft, so a keyway was added to signify the wheel was a "worker and not an idler."
The keyway in the center of the hub is of great significance, because it represents the individual Rotarian member, who is the key factor in every club. Quality members are the keys, needed for the hub to engage with the shaft and turn, putting the energy into motion and creating the power for the gears to do their work.

The Rotary wheel stands for much more than a service club symbol or logo. It represents caring and sharing, friendship and love, plus a commitment with a "you can count on me" attitude. It portrays an "I give more than I take" culture by those who show they care, trying to shine a light of hope on all the despair in dark corners of the world.

The Rotary wheel has been a "magic key" for us, opening doors to special places and unique experiences, including warm hospitality, and yes ...even opening the hearts of many new friends.

Let us use this key... Helping to make the world a better place to live, one friendship at a time.


Monday 26 October 2015

HOW WE CElEBRATED THE 2015 WORLD POLIO DAY

It was a busy and funny day to us.We started by the fundraising car wash with the interactors from Josiah Girls high School and Bukoba secondary school.On the preparations of this day the rotary club of Bukoba prepared the Polio essay competition.SO on this day the winners were announced and the awards were given where the first place winner recived 100000TSH and the second winner Received 50,000TSH.

 Rotaractors happy to be the part of the Rotary end polio campaign

Assistant District Rotaract Representative Miss Ivony Kamala(with a brown tshirt) happy with the Interactors from Josia Girls high school











The President of Rotaract club of bukoba  Busy






 POLIO ESSAY COMPETITION AWARDS GIVEN TO THE INTERACTORS WHO PARTICIPATED IN THE COMPETITION.